Kampeni za Chadema, ni harakati au changamoto kwa jamii?

0

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeanzisha kampeni mbalimbali zinazolenga kuchochea mabadiliko ya kisiasa na kijamii.

Hata hivyo, baadhi ya kampeni hizi zimeibua maswali na wasiwasi mkubwa miongoni mwa wanachama na wadau wa siasa.

Chadema imezindua kampeni ya ukusanyaji wa michango kupitia mpango wa ‘Tone Tone,’ unaolenga kusaidia chama kifedha. Ingawa dhamira inaweza kuwa njema, lakini kuna wasiwasi kuhusu uwazi wa mfumo huu, kwani chama kilishawahi kukumbwa na mgogoro wa fedha mwaka 2013.

Mgogoro huo ulihusisha shutuma za matumizi mabaya ya fedha za chama kati ya viongozi waandamizi, na suala hilo lilisababisha mvutano mkubwa ndani ya chama, ingawa baadaye lilishughulikiwa kwa njia za ndani ya chama.

Chadema pia wameanzisha kampeni ya ‘No Reform, No Election,’ kushinikiza mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi. Hata hivyo, kampeni hii imewapa wanachama wake mkanganyiko, hasa wale wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali.

Baadhi yao wanahisi kuwa chama kimekosa mwelekeo thabiti, jambo linalowakatisha tamaa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi.

Changamoto za vuguvugu za NETO.

Kundi la vijana maarufu kama NETO, likiongozwa na Joseph Kaheza na Daniel Edgar, hawa ni wanachama wa muda mrefu wa Chadema tangu walipokuwa vyuoni, ambapo baadhi yao walihudumu kama viongozi wa Jumuiya za wanachama wa chama hicho ndani ya vyuo vikuu.

Kinachofanyika kwa sasa ni mwendelezo wa mtindo wa vuguvugu la shinikizo zilizopo ndani ya mipango ya Chadema, ni agenda za Chadema ambapo hili ni miongoni, lakini yapo mengine yanakuja. Kitu cha msingi katika mavugu vugu haya jamii inafaidika na nini, ndio jambo la kutafakari.

Baadhi ya wanachama na wachambuzi wanasema harakati hizi si kwa ajili ya maendeleo, bali ni maandalizi ya kujijenga kisiasa na kupitisha agenda binafsi, kupitia majukwaa ya kijamii na jumuiya zinazohusiana na chama. Wananchi wanapaswa kuwa makini na kutafakari kabla ya kushiriki au kutumiwa kwenye mivutano hii ya kisiasa.

Umuhimu wa Mifumo rasmi na uwajibikaji

Ili kuwa chama chenye uimara, Chadema kinapaswa kuweka mifumo madhubuti ya usimamizi wa fedha na uwazi. Historia ya migogoro ya fedha ndani ya chama hicho inaonyesha umuhimu wa mifumo rasmi ili kuepusha migogoro ya baadaye, kama ilivyotokea 2023.

Wananchi wanapaswa kuchunguza kwa makini madhumuni ya kampeni za kisiasa badala ya kushabikia harakati zisizoeleweka. Siasa ni za muda, lakini mshikamano wa jamii ni wa kudumu. Ni muhimu kwa jamii kutumia busara na kutathmini athari za kila kampeni kwa mustakabali wa Taifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here