Kamati ya uchumi yaridhishwa na utekelezaji wa miradi Wilaya ya Kibaha

0

KAMATI ya Uchumi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo kwa robo ya tatu ya mwaka 2024/2025, ikionesha kuridhishwa na hatua zilizofikiwa.

Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni mradi wa kusafisha shamba la pamoja katika kijiji cha Lukenge, ambapo ekari 40 kati ya 53 zimeshasafishwa na ekari 17 tayari zimepandwa zao la ufuta.

Aidha, kamati hiyo ilitembelea ujenzi wa jiko la gesi katika Shule ya Msingi Ruvu JKT, mradi uliogharimu Shilingi Milioni 19.2. Jiko hilo limepunguza gharama za upishi na kuchangia utunzaji wa mazingira kwa kuacha matumizi ya kuni.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Nasikwa Mbwambo, alisema, wanatekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la matumizi ya nishati safi kwa taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100.

Mwenyekiti wa Halmashauri, Erasto Makala, amepongeza juhudi hizo na kuitaka teknolojia hiyo kusambazwa katika shule za pembezoni ili kuokoa mazingira zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here