Na Mwandishi Wetu
MGOMBEA mteule wa Ubunge Jimbo la Kibamba (CCM), Angellah Jasmine Kariuki amechukua fomu ya kuwania nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka 2025.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu na Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Rose Mpeleta, Kairuki alisema yupo tayari kuwatumikia wakazi wa Kibamba pindi akipata ridhaa yao.
Alisema, atafanya kampeni za kistaarabu zenye kuheshimu misingi ya demokrasia na mshikamano wa Kitaifa.