Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imemteua Doyo Hassan Doyo kugombea Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Chausiku Khatib Mohamed kugombea Kiti cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya National League for Democracy (NLD).
Hafla hiyo ya uteuzi iliyofanyika kwenye Ofisi za Tume zilizopo Njedengwa, jijini Dodoma Agosti 27, 2025 imeongozwa na Mwenyekiti wa Tume, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele.