Elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia yatolewa Kibaha DC

0

WAJASILIAMALI wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha wamepata elimu juu ya matumizi ya Nishati safi katika kata zote za halmashauri hiyo.

Akizungumza kwenye mafunzo hayo Emanuel Shirima Mratibu wa Nishati safi wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha, amewataka wajasiriamali kutumia Nishati safi ambazo ni gesi, umeme na Nishati mbadala zinginezo, ili kuepukana na athari za kimazingira, Kiafya na Kiuchumi.

Nae Afisa maendeleo ya jamii Pudenciana Domel aliendelea kutoa elimu hiyo kwa kuelezea athari mbalimbali za matumizi ya nishati isiyofaa,Athari hizo ni kama vile homa ya mapafu, magonjwa sugu ya kikohozi, saratani ya mapafu, macho pamoja na kuongezeka kwa hewa ya ukaa Kwenye uso wa dunia.

Kwa wakati huo huo baadhi ya wananchi wameishukuru Serikali kwa kuwapa elimu juu ya matumizi ya nishati safi na kutoa ombi kwa serikali ya awamu ya sita kupunguza gharama za ununuaji na ujazaji wa mitungi ya gesi ili kila mwananchi awezi kutumia nishati safi.

Hivyo, katika kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hasaan katika matumizi ya nishati safi Halmashauri ya wilaya ya Kibaha itaendelea kuhamasisha na kutoa elimu juu ya matumizi ya nishati safi kwa wananchi na jamii nzima kwa ujumla.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here