Na Albert Kawogo
MGOMBEA kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan ametua Ukanda wa Kilimo leo Jumatano Septemba 3, 2025 na anaanza kampeni katika Mkoa Songwe.
Mkoa huo wa Songwe wenye wakazi 1,344,687 unajihusisha na kilimo cha mazao mbalimbali ikiwemo kilimo cha mahindi.
Akiwa mkoani humo atafanya mikutano katika mji wa Tunduma na Vwawa kwa kuwaomba wananchi ridhaa ya kuchaguliwa katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025
Kazi nyingine atakayoifanya ni kuwanadi wagombea ubunge na udiwani wa chama hicho pamoja na kunadi Ilani ya Uchaguzi.
Rais kupitia Ilani hiyo, ataelezea mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka minne ya uongozi wake pamoja na kutoa ahadi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Hapa ni baadhi ya miradi iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa katika Mkoa huo.
1. Ujenzi wa barabara kuu ya Tanzam kwa njia nne kuanzia Igawa (Mbeya) hadi Tunduma (Songwe) km 218
2.Ujenzi wa barabara ya Ruanda/Iyula (Tanzam Jnct)-Nyimbili-Itumba-Isongole (Malawi Border) km 79.6
3.Ujenzi wa barabara ya Mahenje-Vwawa km 32
- Barabara ya kilomita 130 ya Utambalila-Chitete Bypass
- Makongolosi-Chang’ombe-Mbalizi
6.Isongole-Isoko km 52
7.Ujenzi wa Tunduma Dry Port (Mpemba)
- Miradi wa Uchimbaji Madini Adimu (Ngualla Rare Earth Project)
- Mradi wa uchimbaji dhahabu Wilaya ya Songwe
10.Ujenzi wa Maegesho ya Kisasa ya Malori Chimbuya.
11.Ujenzi wa Vwawa-Mpemba-Nkangamo bypass.
12.Ujenzi wa Chuo cha Mifugo Mbozi
13.Iboya Onestop Inspection Centre
14.Ujenzi wa Makao Makuu ya TRA & TanRoads
15.Ujenzi wa Mradi mkubwa wa Umeme wa Grid ya Taifa kuunganisha na Zambia Mbeya-Tunduma-Sumbawanga kv 400
16.Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe
17.Tawi la Chuo Cha Ufundi DIT Myunga Campus
18.Ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya ya Ileje.
19.Mradi wa Maji Itumba-Isongole
20.Ujenzi wa Chuo Cha VETA cha mkoa
Miradi aliyoikamilisha Rais Samia ndani ya miaka minne ni:-
-Ujenzi wa Hospital ya Mji Tunduma
-Barabara ya Mpemba/Tunduma-Isongole km 50
-Ujenzi wa Makao Makuu ya Wilaya ya Momba, Songwe na Mbozi DC
-Ujenzi wa Makao Makuu ya Mkoa BwawaMiradi ambayo Iko mbioni ‘pipeline’ ni;
-Upembuzi yakinifu wa Vwawa na Tunduma Bypass
-Upembuzi yakinifu wa mradi mkubwa wa Maji kutoka Mto Momba ]adi Tunduma, Bwawa na Mlowo (over 320bln)
-Songwe Airport
-Songwe River Hydropower Project. Miradi hiyo mikubwa itakapokamilika itainua uchumi wa Mkoa wa Songwe na kuleta ustawi kwa wananchi wake na Taifa kwa ujumla.
Dkt. Samia ambaye mgombea wake Mwenza ni Balozi Dkt. John Nchimbi baada kufanya uzinduzi wa kampeni katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe, Dar es Salaam Agosti 28, 2025, tayari ameshafanya mikutano mingine ya kampeni katika mikoa ya Morogoro katika miji ya Ngerengere, Morogoro Mjini, Mvomero, Kilosa, Gairo na Dodoma katika miji ya Kibaigwa, Chamwino, Chemba, Kondoa na Dodoma Mjini.
Kwa mujibu wa ratiba ya kampeni;-
Septemba 4-5, 2025 ataendelea na Mkoa wa Mbeya katika Mji wa Mbalizi na Mbeya Mjini Uwanja wa Ndege wa zamani uliopo eneo la Mwanjelwa.
Siku inayofuata atafanya mikutano Rungwe Mashariki, wilayani Mbarali katika Mji ya Ubaruku na Igawa baada ya hapo ataelekea mkoani Njombe.