Dkt. Mwinyi afungua shule iliyogharimu zaidi ya Bilioni 7

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameifungua Skuli ya Kwanza ya Ghorofa Kisiwani Tumbatu iliyogharimu Shilingi Bilioni 7.015.

Akizungumza na Wananchi baada ya kuifungua Skuli hiyo Rais Dkt.Mwinyi ameziagiza Mamlaka zinazoshughulika na ajira kuhakikisha zinatoa fursa za ajira kwa Vijana wa Tumbatu wenye sifa zinazohitajika.

Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipoifungua Skuli ya Sekondari ya Tumbatu, Wilaya ndogo Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amezitaka Mamlaka hizo katika Sekta za Afya, Elimu , Miundombinu, Maji , Umeme na nyenginezo kusimamia agizo hilo ili miradi iliyomo Tumbatu ilete tìja kwa Wananchi na kuongeza Ufanisi.

Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa Serikali inakusudia kujenga Nyumba za Walimu na Dahalia ili Walimu watakaofundisha katika Skuli ya Tumbatu waishi katika Nyumba hizo.

Rais Dkt.Mwinyi amewahakikishia Wananchi wa Tumbatu kuwa kinaçhofanyika sasa ni Utekelezaji wa Ahadi zake na kwamba zitaendelea kutekelezwa zaidi .

Akizungumzia suala la Utalii ameeleza kuwa Serikali haina nia ya Kupeleka Shughuli za Utalii Kisiwani humo na kuwataka wananchi kuyaepuka Maneno yasio na Ukweli yanayoenezwa na Watu wasiopenda Maendeleo.

“Sina nia ya kuleta Utalii Tumbatu, utalii utapelekwa kwa Watu wanaoutaka sio Tumbatu” alisisitiza Dkt.Mwinyi.

Rais Dkt. Mwinyi amewahimiza Vijana Kusoma kwa bidii kwa lengo la kuongeza Ufaulu kufuatia kuwepo kwa Skuli yenye Viwango vya Ubora ,Maktaba, Maabara ya Kisasa ya Sayansi na Madarasa mazuri.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi ameliagiza Shirika la Umeme kuondoa changamoto ya Kukatika kwa Umeme mara kwa mara tatizo alilolielezea kuwa ni la nchi nzima.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here