Dkt. Abbas aipongeza TAWA kwa kutekeleza maelekezo ya Rais Samia

0

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas, ametembelea Makao Makuu ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), na kuipongeza Bodi na Menejimenti ya taasisi hiyo kwa kutekeleza kwa kasi maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika masuala ya uhifadhi.

Akizungumza na wafanyakazi wa TAWA leo Jumanne Disemba 10, 2024, Dkt. Abbas alisema, Rais alipokuwa ziarani mkoani Ruvuma alitoa maelekezo ya kununuliwa ndege nyuki (drones) zaidi katika kukabiliana na changamoto ya wanyama wakali na waharibifu.

“Leo nimefika hapa na kuambiwa mmeshanunua ndege nyuki mpya mbili na mlishanunua nyingine nne na kufanya idadi ya jumla kwa taasisi nzima na zile za awali kuwa 11. Hili ni jambo kubwa katika kutekeleza maelekezo ya Rais na ni hatua muhimu katika kukabiliana na wanyama wakali,” alisema Dkt. Abbas.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here