CCM yaridhishwa na uongozi wa Dkt. Mwinyi

0

Na Jumbe Abdallah

CHAMA Cha Mapindizi (CCM), kimeridhishwa na uongozi wa Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdulrahman Kinana, katika maadhimisho ya miaka mitatu ya uongozi wa Dkt. Mwinyi.

Kinana alisema, Dkt. Mwinyi amejituma na kujikita katika kuleta maendeleo ya wananchi wa Unguja na Pemba huku akiwaunganisha kuwa kitu kimoja.

Akiyataja mafanikio yaliyopatikana Zanzibar kwa miaka mitatu tangu Rais Dkt. Mwinyi alipoingia madarakani, Kinana alisema ni pamoja na kuharakisha maendeleo kwa kutekeleza miradi mikubwa ikiwemo ujenzi wa shule, hospitali na miradi ya wananchi ya kiuchumi.

Aidha, alisema amewaunganisha wananchi, hivyo kusahau tofauti za itikadi za kisiasa, na watu wote kuwa wamoja.

Kinana aliendelea kusema, hatua hiyo inatoa matumaini katika kipindi cha miaka miwili iliyobakia kufikia ukamilikaji wa malengo ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.

“Rais Mwinyi tunakushuru sana, katika kipindi cha miaka mitatu umefanya mambo makubwa, ikiwemo kuleta mabadiliko makubwa ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi, pamoja na kuwaunganisha wananchi na kuimarisha amani na utulivu wa kisiasa,” alisema Kinana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here