Bunge lapitisha Trilioni 10.125 za TAMISEMI

0

BUNGE limeidhinisha matumizi ya Shilingi Trilioni 10.125 kwa ajili ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Sekretarieti za mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi zake kwa mwaka 2024/25 na kati ya hizo Shilingi Trilioni 3.415 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Fedha hizo zilizoidhinishiwa na bunge zimeongezeka kwa takribani Shilingi Bilioni 900 ikilinganishwa na bajeti ya Shilingi Trilioni 9.18 zilizoidhinishwa mwaka 2023/24.

Pia, Bunge limeidhinishia Ofisi ya Rais – TAMISEMI, taasisi zilizo chini yake, mikoa 26 ikijumuisha halmashauri 184 kukusanya maduhuli na mapato ya ndani ya Shilingi Trilioni 1.60.

Aidha, katika fedha zilizoidhinishwa Shilingi Bilioni 17.79 zinaelekezwa kwa ajili ya kuratibu na kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024,ambapo Shilingi Trilioni 1.02 zitatumika katika kutekeleza shughuli katika sekta ya elimu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here