Bilioni 2.4 zatumika kwenye michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA 2025

0

OR-TAMISEMI

ZAIDI ya Shilingi Bilioni 2.4 zimetengwa na Serikali kupitia Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa mwaka 2025 kwaajili ya Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa shule za Msingi na Sekondari.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Zainab Katimba wakati wa uzinduzi wa Mashindano hayo kitaifa katika viwanja vya Kichangani kata ya Kihesa Manispaa ya Iringa Mkoani Iringa.

“Nitumie nafasi hii kumshukuru sana Mhe.Rais kwa kuendelea kutuwezesha na kutupatia fedha za kutosha kuandaa na kuendesha mashindano haya kila mwaka, jambo ambalo limeendelea kukuza sekta ya michezo nchini,” alisema.

“Michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA imekuwa na mchango mkubwa katika kuandaa wanamichezo wa timu za Taifa ambao wamekuwa wakiliwakilisha Taifa katika michezo mbalimbali” ameeleza Katimba.

Aidha, Katimba alisema kuwa michezo ya shule imekuwa sehemu ya kuimarisha Muungano kutokana na ushiriki wa wanafunzi kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.

Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA inafanyika Mkoani Iringa, ikiwa ni zaidi ya miaka 30 tangu yalipofanyika kwa mara ya mwisho Mkoani humo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here