Balozi Kasike, FRELIMO wajadili uhusiano wa Tanzania na Msumbiji

0

BALOZI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji Phaustine Kasike, amekutana na Alcinda António de Abreu, Mjumbe wa Kamisheni ya Siasa ya Chama cha FRELIMO.

Kupitia mkutano huo uliofanyika kwenye Ofisi za Makao Makuu ya FRELIMO zilizopo jijini Maputo, Viongozi hao wawili walizungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji na kukubaliana juu ya umuhimu kwa uhusiano huo kuendelezwa kwa maslahi ya nchi hizo mbili.

Kwa upande mwingine, Balozi Phaustine alikipongeza Chama cha FRELIMO kwa kumaliza mchakato wa kumpata Mgombea wake wa nafasi ya Urais kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 9, 2024 ambapo Daniel Francisco Chapo aliteuliwa kupeperusha bendera ya Chama hicho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here