WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amesema Wizara yake imepanga kutekeleza vipaumbele 14 katika mpango wa bajeti wa mwaka 2025/26.
Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa wizara na taasisi zake kwa mwaka 2025/26, Mchengerwa alisema utekelezaji wa mpango wa majeti unazingatia vipaumbele vya kusimamia shughuli za utawala bora, kukuza demokrasia, ushirikishwaji wa wananchi na Ugatuaji wa Madaraka kwa Umma (D by D).
Pia, kuratibu na kusimamia utekelezaji wa shughuli za utoaji wa huduma za jamii, kuratibu na kusimamia mkakati wa kuongeza ukusanyaji wa mapato na kudhibiti matumizi yasiyo na tija katika ngazi zote na kufanya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mikoa, mamlaka za serikali za mitaa na taasisi zinazosimamiwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI.
Mchengerwa alisema, kufanya uratibu wa usimamizi wa mifumo ya TEHAMA, kuendeleza rasilimali watu katika ngazi zote za Ofisi ya Rais – TAMISEMI, kuratibu na kusimamia shughuli za kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa watumishi wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, mikoa na mamlaka za serikali za mitaa na kuratibu na kushiriki michezo ya shule za msingi (UMITASHUMTA), sekondari (UMISSETA) na mashindano ya michezo ya shule za sekondari za Afrika Mashariki.
Alisema, kuratibu shughuli za utendaji wa kazi wa taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI, kuratibu na kusimamia ujenzi wa miradi ya maendeleo katika ngazi zote za Ofisi ya Rais-TAMISEMI, kuratibu uibuaji wa miradi ya kimkakati na miradi inayopaswa kutekelezwa kwa ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi katika mamlaka za serikali za mitaa na kusimamia na kuratibu shughuli za utunzaji wa mazingira na uhifadhi wa maliasili katika mikoa na mamlaka za serikali za mitaa.
Kipaumbele kingine ni kuratibu na kusimamia utekelezaji wa afua za mabadiliko ya tabianchi ikiwa ni pamoja na uendelezaji wa utalii, uhamasishaji wa nishati