Waziri Masauni azindua mradi wa ‘RESOLVE’

0

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Yusuf Masauni amezindua Mradi wa Suluhisha ‘RESOLVE’ ambao unalenga katika utunzaji wa vyanzo vya maji, misitu na maeneo yanayohusika na shughuli za kilimo.

Mradi huo unaotekelezwa na Shirika la Kimataifa la Hifadhi ya Mazingira utatekeleza katika mikoa ya Morogoro na Iringa kwa muda wa miaka mitatu.

Sanjari na kuzindua mradi huo Waziri Masauni amefunga warsha ya wadau wanaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Norway (NORAD) linalohusu uhusiano uliopo baina ya Mabadiliko ya tabianchi na kilimo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, alisema Ofisi ya Makamu wa Rais itaendeleza dhamira yake ya kuunga mkono sera na programu zinazokuza kilimo endelevu na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Pia, Waziri Masauni alisema Ofisi hiyo itaendelea kufanya kazi kwa karibu na wadau wote ili kukusanya rasilimali, kuimarisha uwezo na kuleta mabadiliko yenye matokeo na kufanikiwa kwa miradi iliyopo na mipya itakayoonesha dhamira katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here