RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Udaktari ya Heshima (PhD) katika uongozi, leo tarehe 24 Novemba 2024, kwenye mahafali ya 23 ya Chuo Kikuu cha Mzumbe, yaliyofanyika Kampasi Kuu ya Morogoro.
Shahada hiyo aliyotunukiwa Rais Dkt. Samia, imetokana na umahiri na uwezo aliouonesha kwenye uongozi katika nafasi mbalimbali alizotumikia kupitia Chama, Serikali na nje ya hapo.
Pia, Dkt. Samia leo Novemba 24, 2024 ni mgeni maalum kwenye mahafali hayo yanayofanyika katika Viwanja vya Maekani.