‘Wazazi tuone aibu mtoto akikatishwa masomo’

0

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Buteko amewataka wazazi na walezi nchini kuhakikisha wanafunzi wanafikia malengo bila kukatisha masomo huku akiwahimiza Wanafunzi kote nchini kuzingatia masomo kwani ndio fursa pekee ya kupata maarifa.

Dkt. Biteko ametoa wito huo katika uzinduzi wa shule ya sekondari kidato cha kwanza hadi cha sita ya Miles and Kimberly White iliyopo Kata ya Mapatano wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga yenye uwezo wa kubeba wanafunzi 736 na imegharimu
kiasi cha shilingi Bilioni 12 cha ujenzi kwa ufadhili wa Abbott Fund.

“Nawaomba wazazi muone aibu kuona watoto anaishia njiani kwasababu tu anataka kuharakia maisha wakati kwa vyovyote vile atayakuta kwa mfano watoto wa kike kuachishwa shule kwaajili ya kiwahi ndoa jambo ambalo wewe unayetaka kuoa unatafuta jela na aibu” alisema.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi – TAMISEMI Mohamed Mchengerwa, Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI Zainab Katimba alisema TAMISEMI inaendelea kushirikiana na wadau mbalibali wa ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha kunakuwepo na mazingira rafiki ya kujifunza na kujifunzia ili kuboresha Elimu nchini.

“Ofisi ya Rais – TAMISEMI ni jukumu letu kuhakikisha uwepo wa miundombinu rafiki na ya kutosha ili watoto wetu wote wenye umri wa kwenda shule waandilishwe na wale waliofaulu wajiunge na masomo ya sekondari na kwa Kutimiza adhima hii tumeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuweka mazingira rafiki ya kujifunzia na kufundishia ili wanafunzi wote wakamilishe mzunguko wao wa Elimu bila vikwazo vyovyote” alisema Katimba.

Aidha, Katimba amemshukru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu kwa ujenzi wa shule na kutoa ruzuku kwa shule zote ikiwemo Elimu bila ada na mpaka kufikia Juni 2024 amefanya uwekezaji wa jumla ya Shilingi Trilioni 3.43 kuhudumia nchi nzima katika sekta ya elimu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here