Ujio wa Meli ya kitabibu ni faraja kwa Watanzania – Kijavara

0

NAIBU Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Juma Kijavara amesema, ujio wa Meli ya Kitabibu ya Kikosi cha wanajeshi wa Majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA), “Peace Ark” ni faraja kwa Watanzania wanaohitaji msaada wa matibabu.

Kijavara alisema hayo wakati akipokea msafara wa Maafisa wa Kijeshi waliokuja na meli hiyo, uliotembelea Makao Makuu ya TPA kwa ajili ya kujitambulisha (Courtesy Call), ambapo alishauri huduma hiyo iwafikie pia Watanzania walioko nje ya Jiji la Dar es Salaam.

Kwa upande wake kiongozi wa Msafara wa Maafisa hao wa Kijeshi Kamanda Zhang Yi alisema, Wataalamu waliopo Melini watatoa huduma za bure za tiba na uchunguzi wa afya ili kudumisha ushirikiano ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya ushirikiano kati ya Tanzania na China.

Alisema, ushirikiano huo wa Kihistoria wa Mataifa ya Tanzania na China utaendelea kuimarishwa kupitia shughuli za Sekta mbalimbali zenye kugusa maisha ya Watu na ustawi wa kiuchumi wa Mataifa haya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here