Na Habib Miradji
MOJAWAPO ya mahitaji ya lazima kwa binaadam ni chakula, mavazi na makazi. Mahitaji haya yalitajwa toka kupatikana kwa uhuru wa nchi yetu mwaka 1961. Lengo kubwa la taifa kuwapatia chakula bora ili wawe na afya njema, makazi bora yenye staha na ya kulinda mazingira na mavazi
Ujenzi wa nyumba bora za kisasa ulikabidhiwa Shirika la Nyumba (NHC) Kutokana na mazingira yaliyokuwepo wakati huo, Shirika hili lilianza kuboresha nyumba nyingi za wakazi wa mijini na kuifanya kaulimbiu ya “Tunalijenga taifa” kutamalaki kwa awamu zote za utawala wa nchi yetu
NHC ikaanza kazi hiyo kabla ya Azimio la Arusha, ambapo wananchi wengi walijengewa nyumba na shirika na baadae kuuzwa kwao. Misingi ya ujengaji nyumba na kuuzwa na nyingine kupangisha nyumba kwa wafanyakazi kulisukuma maendeleo ya upatikanaji wa makazi bora.
Baada ya Azimio la Arusha baadhi ya nyumba zilizotaifishwa zilikabidhiwa kwa NHC na nyingine kwa Msajili wa Majumba. Kazi ya kujenga nyumba bora kwa wananchi ikapungua kutokana na shirika kuzidiwa na kazi za matunzo na ukarabati wa nyumba zilizotaifishwa.
Mbali na kushughulika na upangishaji wa majumba yaliyotaifishwa, NHC iliweka alama ya kujenga nyumba kila wilaya na kuzipangisha kwa wafanyakazi na wafanyabiashara. Mahali pengine hata wakulima mfano Tarime mkulima alijengewa nyumba za makazi yeye na familia yake.
Athari ya vita vya Kagera na mabadiliko ya uchumi kutoka kwenye ujamaa hadi kwenye Uchumi wa soko (huria) uliyumbisha mashirika yya umma likiwemo shirika la nyumba badala ya utaifishaji, mwelekeo mpya ukawa ubinafsishaji kuruhusu watu wenye mitaji kuwekeza mitaji yao.
Katika kupunguza mashirika yanayotia hasara, Serikali ilifanya maboresho. Nyumba zilizomilikiwa na Msajili wa Majumba zilikabidhiwa kwa NHC. Majukumu mapya ya shirika hilo ni kuanza kutumia mitaji ya wawekezaji wa ndani kwa kuendesha miradi ya pamoja kati ya wazalendo na shirika.
Mageuzi haya yalianza kubadili sura ya miji mikubwa mbalimbali katika nchi yetu majumba ya kibiashara na makazi ya kisasa yenye teknolojia mpya. Soko la Real Estate likapanuka na pia kupata ushindani kutoka kwa waendelezaji binafsi na mashirika megine ya umma dhidi ya NHC
Wakazi wa Kigamboni hivi karibuni walishuhudia NHC na Shirika la hifadhi ya Jamii (NSSF) wakichuana kujenga nyumba na kuziuza kwa walio na uhitaji wa kununua nyumba. Uzoefu wa NHC katika biashara ya kujenga na kuuza nyumba ulichangia mradi kupata faida kubwa.
Uamuzi wa serikali kuhamia Dodoma,uliipatia Changamoto mpya NHC Mojawapo ni kuyakabidhi baadhi ya majengo iliyokuwa inayatumia kwa NHC pia kusimamisha baadhi ya miradi iliyoanza kutekelezwa na NHC kwa lengo la kutathmini upya mwelekeo wa shirika katika awamu zijazo.
Mwelekeo huu mpya uliibua kuzaliwa kwa majengo mapya yaliyokamilishwa awamu hii ya sita ya utawala wan chi yetu. Baadhi ya majengo hayo kwa ajili ya makazi na biashara katika jiji la Dar es Salaam Victoria Plaza, Eco Residence, Kigamboni Housing Estate, Mwongozo Housing Estate, Mindu plaza na Mchikichini residentials Apartments.
Jijini Arusha miradi ya Medali, Levolisi na Meru Residential Apartment imekamilika na nyumba zimeanza kuuzwa. Mradi wa Meru Residential Apartment zimenunuliwa zote. Hali hii imeifanya manejimenti ya NHC kuwa kinara wa kuendeleza miliki ya makazi na majengo ya umma.
Miradi mingine iliyokamilika ni nyumba 5000 za bei nafuu, jengo la biashara la rahaleo na lile la 2D Katika ziara ya hivi karibuni ya wabunge wa kamati ya kamati ya kudumu ya Bunge ya uwekezaji wa mitaji ya umma (PIC) walivutiwa na uwekezaji huu unaoendana na dira ya taifa.
Jiji la Dar es Salam, litakuwa na maandhari mapya NHC kukamilika kwa Miradi ya Samia Housing Scheme, Morroco Square Apartments, na 711 eneo la Kawe. Nako Arusha italigeuza jiji hilo baada ya kukamilika kwa mradi wa Safari city. Dodoma pia Mradi wa Iyumbu nyumba 1000.
Wakazi wa Bombambili (Geita), Ilembo (Katavi), Kongwa {Mpwapwa}, Mkinga (Tanga), Mkuzo (Ruvuma), Mlole (Kigoma), Mrara (Manyara) Mtanda( Lindi) Mvomero (Morogoro) na Unyakumi (Singida} wameingia katika kaulimbiu ya NHC ya “Nyumba yangu, maisha yangu” ambapo nyumba zilizokamilika kwenye maeneo yao zinauzwa kwa bei nafuu.
Kuna miradi ya Mkakati iliyotekelezwana NHC kuanzia mwaka 2021 hadi leo. Miradi hiyo tayari na huduma zimeanza kutolewa miradi hii ni Pamoja na Mkendo phase II (Musoma), Soko la Mutukula (Kagera), Mradi wa Maduka(Singida mjini) na Mtaa wa Rwegasore jijini Mwanza
Miradi mingine ni wa Nyumba 1000 Chamwino (Dodoma), Ujenzi wa jengo Mkuu wilaya ya Malinyi (Morogoro) na Halmashauri ya wilaya za Wanging’ombe(Njombe) na Hai (Kilimanjaro), Pamoja na Machinjio ya kisasa eneno la Vingunguti (Ilala) hapa jijini Da es salaam.
Katika kuunga mkono jitihada za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika sekta ya Afya NHC imefanikisha kujenga hospitali kuu ya Rufaa ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kwangwa Musoma na ile ya Mitengo (Mtwara) na Makao Makuu Mamlaka ya Madawa (TMDA).
Miradi mikakati iliyotekelezwa na shirika la Nyumba la taifa ni ujenzi wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA) Dodoma na Ofisi za Wakala wa Misitu Mkolani Mwanza Kilimanjaro, Iyondoswima (Songwe), Mlele (Katavi) Mbeya, Lushoto (Tanga), Ruvuma Mvomero, Mtibwa, na Uluguru (Morogoro).
Hivi karibuni, Shirika la Nyumba la Taifa na waendelezaji 270 wa miliki za makazi wameingia mkataba wa kuvunja majengo 16 na nyumba 190 kupisha ujenzi wa majengo mapya ya ajili ya biashara na makazi. Uwekezaji huu utaendelea kulifanya shirika hili la umma kuwa kinara wa mabadiliko ya maendeleo.
NHC ni wawekezaji wakubwa wa ndani wanaotoa huduma ya kuboresha makazi yanaendana na zama mpya na za kisasa. Mbali na kuchangia pato la taifa, umebadili maandhari na mazingira mapya. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) katika ziara yaimeishauri serikali kulipatia fedha kuwekeza katika Miliki zenye faida.