Maandalizi ya CHAN 2024 na AFCON 2027 yaanza

0

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro ameongoza kikao cha kujadili maandalizi ya Fainali za Mashindano ya CHAN mwaka 2024 na AFCON 2027 yatakayofanyika nchini Tanzania kwa kushirikiana na Kenya na Uganda kilichofanyika Mei 6, 2024 Jijini Dodoma.

Kikao hicho kimejadili ukarabati wa miundombinu ambayo itatumika katika mashindano hayo iliyopo Tanzania Bara na Zanzibar kwa kuzingatia mapendekezo yaliyotolewa na Wakaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Kikao hicho kimehudhuriwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Tabia Maulid Mwita, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Fatma Hamad Rajab, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Suleiman Serera, baadhi ya watendaji wa wizara na viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakiongozwa na Rais wa Shirikisho hilo, Wallace Karia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here