Habari Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano By Ripota Wetu - April 26, 2024 0 FacebookTwitterPinterestWhatsApp Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam wakati wa Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Aprili, 2024. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wa Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Sherehe hizo zimefanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Aprili, 2024. Viongozi mbalimbali wa serikali wakishiriki sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizofanyika katika Uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Salaam leo Aprili 26, 2024.