RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametangaza kwamba, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi maarufu kama ‘Mzee ruksa’ amefariki dunia katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam.
Mzee Mwinyi ambaye aliingia madarakani Novemba 5, 1985, alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya Mapafu.
“Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi, amekua akipatiwa matibabu tangu Novemba mwaka jana nchini Uingereza, na baadaYe kurejea nchini alipokua akiendelea na matibabu katika hospitali ya Mzena, hadi umauti ulipomfika,’’ alisema Rais Samia na kuongeza kuwa, Tanzania itaombeleza kwa siku saba.