Serikali yakaribisha wawekezaji Msomera

0
Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi.

Na John Mapepele 

SERIKALI imesema wawekezaji wa ndani na nje wanaruhusiwa kuwekeza katika eneo la Msomera ili kuleta maendeleo na  kusaidia kuboresha maisha ya wananchi walioamua kwa hiari kuhamia  eneo hili.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi ametoa kauli hiyo Kijijini Msomera kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari zaidi ya 60 waliokuwa kwenye ziara maalum ya siku nne  kwenye Hifadhi ya Ngorongoro na Msomera kushuhudia zoezi  linalofanywa na Serikali la kuwahamisha wananchi kwa hiari kupisha uhifadhi na kuwaboreshea maisha yao.

Waandishi wamepomgeza jitihada zinazofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt, Samia Suluhu Hassan za kuwaboreshea wananchi maisha.

Matinyi amewahakikishia wawekezaji kuwa wanaruhisiwa  kuwekeza  kama ambavyo wanafanya katika maeneo mengine kwa kuzingatia sheria za nchi huku pia akiwataka  wananchi kuchangamkia fursa  hizo baada ya jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali za kukamilisha huduma za kijamii na miundombinu yote muhimu.

Alisema, sasa tayari ujenzi wa  nyumba 1000 upo katika hatua mbalimbali kwenye eneo la Msomera na kwamba huduma  za ujenzi wa shule za msingi na sekindari, zahanati,  eneo la mnada, mabwawa ya kunyweshea mifugo, majosho barabara na umeme unafanyika kwa kasi kubwa.

Alisisitiza kwamba, malengo makubwa ya zoezi hili ni kuboresha maisha ya wananchi waliokuwa wakiishi Ngorongoro kwa dhiki na kuboresha uhifadhi wa Ngorongoro kwa faida ya  vizazi vya sasa  na baadaye.

Wakati huo huo alisema, tayari kaya 72 zenye jumla ya watu 500 waliojiandikisha kuhama kwa hiari kutoka Ngorongoro kuja Msomera wanatarajiwa kuagwa kesho katika ofisi za Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na  viongozi mbalimbali wa Serikali.

Katika ziara hiyo waandishi wa Habari iliyoratibiwa na Wizara ya Maliasili kupitia Ngorongoro kwa kushirikiana na  Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali waandishi walipata fursa ya kutembelelea eneo la makazi ya watu Ngorongoro Kisha Msomera.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here