Daraja la BibiTiti kujengwa Muhoro – Rufiji

0

Na Ali Ndaro

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mohamed Mchengerwa ameweka jiwe la msingi ujenzi wa daraja la Bibititi Mohamed, Mohoro-Rufiji lenye urefu wa Mita 80 na kina cha Mita 8.9 kutoka chini hadi juu usawa wa mto, ujenzi wa boksi kalavat mbili pamoja na ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa Kilomita moja.

Hafla hiyo imefanyika kwenye Mohoro wilayani Rufiji hivi karibuni na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali kutoka ngazi ya Wizara na TARURA Makao Makuu.

Baada ya kusainiwa mkataba huo Mchengerwa alisema Fedha za ujenzi wa darahja hilo ni nyingi sana ukilinganisha na mahitaji makubwa ya ujenzi wa Miundombinu nchini hivyo amewataka TARURA kusimamia kazi hiyo kwa weledi na kwa kuzingatia masharti ya Mikataba na kuhakikisha kazi inakamilika kwa wakati na kwa ubora ulioanishwa kimkataba (control on time overrun & poor quality works).

Pia, amewataka TARURA Kuepuka kuongezeka kwa gharama wakati wa utekelezaji na Kuzingatia vipengele muhimu vya mikataba vinavyotaka Makandarasi kuwasilisha dhamana za malipo na dhamana ya utendaji ili kuiepusha Serikali kupata hasara pale mkandarasi anaposhindwa kukamilisha kazi.

‘Niwatake kuhakikisha kuwa nyaraka halali za dhamana kwa ajili ya malipo ya awali zinawasilishwa, dhamana za utendaji kazi na kufuatilia pale zinapomaliza muda wake wakati muda mradi haujakamilika zihuishwe’ amesema Mhe. Mchengerwa.

Halkadhalika amewataka kutumia ujenzi huo kwa ajili ya mafunzo ya Wahandisi chipukizi ili kuwajengea uwezo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi kama hiyo baadae

Akizungumza katika hafla hiyo Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff alisema, Makisio ya gharama za mradi huo wa ujenzi unategemewa kugharibu takriban Shilingi Bilioni 11.5 ambapo muda wa utekelezaji wa mradi huo unategemewa ukiwa ni miezi 18 kwakutumia fedha za mapato ya ndani.

Mkataba huo umesainiwa baina ya mkandarasi mzawa Mac contractor na Wakala wa barabara za mijini na vijijini (TARURA)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here