Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhwani Jakaya Kikwete ametoa wito kwa watumishi wote wa umma nchini kujipanga vizuri na mabadiliko ya Teknolojia hususani matumizi ya akili unde.
Alisema hayo wakati aliposhiriki ufunguzi wa Mkutano wa Maafisa Tawala na RasilimaliWatu Afrika uliofunguliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika Hotel ya Verde, Zanzibar.
Mkutano huo uliohudhuriwa na Maafisa Tawala na RasilimaliWatu takribani 1,220 umelenga kujadili nafasi ya utumishi na ulinzi wa Rasilimali watu katika kipindi hiki cha mabadiliko ya Teknolojia ususani matumizi ya Akili Unde.
“Nina toa wito kwa watumishi wote wa umma kujipanga vizuri na mababiliko haya na wayachukue kama chachu kuimarisha Usimamizi na ukuaji wa Rasilimali Watu, ” Kikwete alisema.