π Bilioni 17 zimetolewa kwa mkandarasi CCCEC
π Bilioni 40 kwa ajili ya kusambaza taa za barabarani
WAZIRI wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amesema Serikali imetenga Shilingi Bilioni 40 kwa ajili ya kusambaza taa za barabarani katika miji ya Dar es Salaam na Arusha, zitakazohudumia Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON 2027).
Akizungumza Aprili 15, 2026 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hoja kwenye Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Ulega amesema maandalizi ya AFCON 2027 yanaendelea vizuri na kuwataka Watanzania kuondoa mashaka.
Aidha, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Shilingi bilioni 17 kama malipo ya awali kwa mkandarasi CCCEC, ambaye tayari ameanza maandalizi ya ujenzi wa barabara inayoelekea Uwanja wa Dkt. Samia Suluhu Hassan uliopo Arusha Mjini.
βTuna furaha kubwa katika Mkoa wa Arusha. Keshokutwa tutamwona Mheshimiwa Waziri Mkuu akizindua ujenzi wa barabara kutoka Mbauda hadi Losinyai. Hii ni ishara kuwa Serikali imejipanga vyema kwa ajili ya michuano hiyo,β ameeleza Ulega.