‘Msingi wa maendeleo ya taifa letu ni watu wenye ujuzi, ubunifu, na maadili’

0

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuhakikisha Tanzania inakuwa na nguvukazi yenye ujuzi wa kisasa na inayoweza kushindana katika soko la ajira la kikanda na kimataifa.

Amesema lengo ni kuhakikisha nguvu kazi hiyo inakuwa na mchango katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Amesema hayo leo Jumamosi (Oktoba 11, 2025) wakati alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ufunguzi wa Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lilizofanyika katika ukumbi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

“Mafanikio ya taifa letu katika miaka ijayo yatategemea kwa kiasi kikubwa ubora wa watu wake. Msingi wa maendeleo ya taifa letu ni watu wenye ujuzi, ubunifu, na maadili. Tuweke mbele elimu bora, ujuzi, ubunifu, na uzalendo kama silaha za kujenga taifa lenye ustawi, amani, na maendeleo jumuishi.

Amesema kuwa katika kuhakikisha Tanzania inaandaa nguvu kazi imara imetekeleza mipango mbalimbali ikiwemo kuanzisha Programu za Elimu ya Ufundi na Ujuzi (VET na TVET) kwa kupanua wigo wa vyuo vya VETA katika kila Wilaya na kuongeza idadi ya wanafunzi wanaopata mafunzo ya vitendo.

“Pia, Serikali imeanzisha Programu ya Taifa ya Maendeleo ya Ujuzi (National Skills Development Programme) inayolenga kujenga ujuzi kwa vijana katika sekta za kilimo, viwanda, teknolojia, nishatina huduma”.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here