BALOZI wa Tanzania nchini Sweden, Mobhare Matinyi amekutana na wanafunzi wapya wa Tanzania waliokuja kusoma shahada za uzamili katika fani mbalimbali nchini Sweden katika muhula wa mwaka 2025/26.
Balozi Matinyi aliwaandalia wanafunzi hao hafla fupi katika makazi yake jijini Stockholm, Jumapili Septemba 21, 2025 ili kuwaeleza umuhimu wa kutumia maarifa na fursa waliopata kwa faida ya taifa.