Dkt. Abbasi akagua Miundombinu ya Kisasa ya Utalii Hifadhi ya Nyerere

0

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, Agosti 8, 2025, amekagua uwekezaji mkubwa wa miundombinu mbalimbali ambayo Serikali imewekeza kufungua utalii Hifadhi ya Taifa Nyerere.

Akiwa Hifadhini hapo amekagua ujenzi wa geti la kuingilia na kutokea abiria, nyumba za kisasa za kulala wageni, maeneo ya wageni kuweka kambi (tented camps) yenye miundombinu yote ikiwemo vyoo na majiko ya kisasa na eneo mahsusi pembeni mwa Mto Rufiji la kupumzikia watalii.

โ€œNimefarijika kuona sehemu kubwa ya miundombinu hii imekamilika na iko tayari kuanza kutumika,โ€ alisema Dkt. Abbasi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here