Wasira: Kwa kazi kubwa aliyoifanya Dkt. Samia, anastahili kuchaguliwa tena

0

Na Mwandishi Wetu, Babati

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Stephen Wasira amesema wakati wanamuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya Chama Dk. Samia Suluhu Hassan, Watanzania ni mashahidi wa kazi kubwa aliyoifanya katika miaka minne na nusu ya uongozi wake.

Akizungumza leo Septemba 1, 2025 katika kikao cha ndani kilichohusisha viongozi na wana CCM Wilaya ya Babati Wasira amesema kwa kuwa tangu Rais Samia amechukua uongozi kutoka kwa mtangulizi Hayati Dkt. John Mafuli kuna mambo makubwa yamefanyika nchini.

“Wanataka kumuondoa lakini sababu hawana na ukisema nao wapinzani pembeni wanasema lakini nyie wakubwa, mmefanya mambo mengi. Nilikuwa mjumbe wa Kamati iliyoandika Ilani mpya ya mwaka 2025-2030 akanipigia kiongozi mmoja wa chama cha upinzani anasema nimeisoma Ilani yenu mmeandika kila kitu sasa sisi tutaandika nini?

“Kwasababu CCM tulikuwa na Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2020 imetekelezwa mpaka tumevuka mpaka na ushahidi wake hata hapa Babati upo katika sekta zinazohusu watu.Tumejenga zahanati 19 , vituo vya afya 8, tumejenga hospitali mbili moja ya kukarabati lakini kama imejengwa upya.

Amefafanua kwani wanaume wameshazoea mfumo dume mpaka urais wanauhusisha na mfumo dume utafikiri kila mwanaume anaweza kuwa Rais.

Hofu nyingine ilikuwa inajengwa tu na nyingine ni ya mazoea lakini Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kazi aliyoachiwa akaweka maneno mawili anakwambia Kazi Iendelee.

‘’Na sisi Tanzania tunataka kuthibitishia Dunia, kwamba kwanza sisi tunaamini katika usawa wa binaadamu na binadamu sote ni sawa wakiwemo kina mama, kwahiyo chama chetu ambacho kikubwa kimemuweka  Samia Suluhu Hassan Mwenyekiti tiketi, kazi ya chama chetu ni kuuza tikrti ambayo inaongozwa na Mwana mama na kuhakikisha anashinda tena kwa kura nyingi’’.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here