Mradi wa ujenzi wa minara 758 wafika asilimia 84.43

0

MRADI wa ujenzi minara 758 unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kushirikiana na kampuni za simu nchini, umefika asilimia 84.43.

Makampuni yanayoshiriki kutekeleza mradi huo wenye thamani ya Shilingi Bilioni 126, ni Airtel, Halotel, Honora (YAS), TTCL na Vodacom.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka UCSAF, hadi kufikia jana, Agosti 1, 2025 minara 640 imekamilika na imeanza kutoa huduma, huku kazi ya kukamilisha minara iliyosalia ikiendelea kwa kasi.

Serikali inatekeleza mradi huu mkubwa unaolenga kuwafikia wananchi Milioni 8.5 wa maeneo ya vijijini ambao watafaidika na huduma za mawasiliano mara mradi utakapokamilika.

Mradi huu ni sehemu muhimu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita, kuboresha upatikanaji wa huduma za mawasiliano na kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata fursa ya kuunganishwa na dunia kupitia huduma za simu na mtandao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here