Serikali yapunguza VAT kwa walipakodi wa mifumo ya Kidigitali

0

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Emmanuel Tutuba amesema Serikali imewapunguzia gharama walipa kodi (VAT) kwa mifumo ya kidigitali kwa 2%.

Tutuba amesema hayo katika Siku ya Visa (Visa Day) iliyoambatana na uzinduzi wa Ofisi ya Kampuni ya Visa nchini Tanzania na kusema kuwa wateja wote wanaolipa kodi kwa kutumia mifumo ya kidigitali kulipa 16% na wale wote wanaolipa kwa fedha taslim watalipa kwa asilimia 18 kama ilivyokuwa awali kuanzia Julai 1, 2025.

Alisema, Serikali imeweka utaratibu huu ili kurahisisha huduma za malipo na kuwavutia zaidi watu wote kutumia zaidi mifumo ya kidigitali katika kufanya miamala badala ya kutembea na pesa taslim.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here