Na Habib Miradji
TUNAJITAYARISHA kuingia kwenye Uchaguzi Mkuu 2025. Mikikimikiki ndani ya vyama vya siasa vya upinzani imeanza kuikabili CCM. Wapinzani wanaichokoza CCM kwa kudai vyama vyao vina demokrasia pana ambayo inatakiwa kuigwa na CCM. Hoja yao kuuteka umma wa Watanzania kuwaunga mkono wawachague.
Wapinzani toka waliporuhusiwa kushiriki kwa vyama vingi vya siasa, historia kamwe haijawaacha salama. NCCR mwaka 1995, CUF na ACT Wazalendo 2017. CHADEMA nao wanapita njia hiyo hiyo baada ya kujiimarisha, uzoefu unaonesha wanabomoa vyama vyao na kuisingizia kuwa CCM inahusika kuvibomoa.
Wakati CCM inafanya mkutano mkuu maalum, kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara ni vyema kwa wajumbe wa mkutano huo wakatafari na kumwona Mwenyekiti wao Dkt Samia ni mwanademokrasia na muumini safu itakayopangwa na chama ndio msingi wa kupata viongozi bora muda wote
Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara huwa ndiye huongoza Kamati ya maadili na kupendeza majina ya wagombea kwa ajili ya vikao vya maamuzi, hivyo kukamilika kwa mkutano huu muhimu unalenga si kukuza demokrasia, bali pia kukiimarisha na hivyo wajumbe wa Mkutano huo watimize wajibu uliofikishwa na Mwenyekiti wao.
Wapinzani wa CCM wana hoja mbili kubwa, hoja ya kwanza ile ya Muungano; vyama vya ACT Wazalendo na Chadema vimeshikilia bango hili. Wameshindwa kuona Muungano ni tunu iliyoasisiwa na vyama mama TANU/ASP iliyozaa CCM. Muungano ni mtoto wa CCM. Wenye kuhubiri utengano hawana budi kupuuzwa.
Wako wapi makada wa CCM wanapoona manufaa yalitokana na muungano hayasemi hadharani? CCM ina mengi ya kusema na kuonyesha Muungano ulivyoleta tija ustawi wa Watanzania wa bara na visiwani wasinyamaze kimya. Waswahili husema mkataa wengi ni mchawi, wapinzani hawana jema na hili.?
Hoja ya pili ya wapinzani kwa kila upande iwe bara au visiwani ni kuwafitinisha Watanzania na CCM, wanadai kuwa imechangia kuwafanya masikini. Ni wakati vyama vya siasa kutengeneza ilani na kuzinadi ili zipimwe na wananchi. Watanzania ni wanaelewa hawataki siasa za maneno matupu majukwani.
Nionavyo, CCM imerahishiwa mno kazi yake. Kama ilivyo ada yake inalazimika wapitie upya ilani na kukabidhi kada wake Dkt. Samia Suluhu Hassan kulisukuma kwa miaka mingine mitano; ana uwezo, nguvu na ari. Hakuna haja ya CCM kuanzisha ya mchakato wa kumpata mwanaCCM atae mzidi Dkt. Samia kwa sasa.
Taifa linamhitaji Dkt. Samia kuliko mtu yeyote kwa kuwa amefanikiwa kututoa kwenye Awamu ya Sita, ambapo makundi mbali mbali yalihitaji uponaji mpya. Wapo wapinzani walienda uhamishoni wamerudi na kuendelea na kazi zao wanaCCM waliojitenga na siasa ambao wamewarudisha kufanya kazi zao upya
Wafanyabiashara na watendaji wa Serikali walipoteza mali zao, na kukaa magerezani nao waliachiwa. Baadhi ya wafanyakazi wa ngazi za chini nao walipoteza ajira zao na mafao sasa wamelipwa. Maono mpya ya Rais Samia kama lilivyo jina la baba yake, ameleta suluhu kwa makundi yaliyoathirika.
Wakulima wa korosho nao walikuwa wahanga, lakini ndani ya kipindi kifupi bei mpya imewanufaisha na kuponywa majeraha. Dkt. Samia toka aingie madarakani amefanikiwa kutibu nyoyo zilizojeruhiwa kwa ujasiri wake; simwoni mwingine wa kumpiku. Ujasiri na uthubutu ameonesha ni kiongozi shupavu kwa wakati huu.
Rais Samia ameonesha ni Uungwana kwa kutembea kwenye kauli zake za tumeona kazi Reconcilition, resilience, reform na rebuild ni Dkt Samia pekee mwenye Kauli mbinu hiyo ndiye anayepaswa kuendelea na kazi CCM haipaswi kutupa kukitupa kisahani cha dhahabu kilicholetewa kwenye mikono ya wajumbe.
Miradi ya kimkakati kama vile ujenzi wa Reli ya SGR unaendelea kwa kasi kubwa, bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere lililopo kwenye hatua za mwisho; kazi yake imewavutia wakazi Afrika ya Mashariki. Naweza kusema katika ukanda wetu huu, Dkt. Samia amekuwa kiongozi mwenye mvuto anaye kubalika na majirani.
Serikali ya Dkt. Samia imekamilisha kila mahali miradi ya elimu, afya, maji, miundombinu vifaa tiba kwenye mahospitali yetu na zahanati vimenunuliwa. Uchumi mkubwa chini ya Rais Samia umeendelea kuimarika, thamani ya dola za kimarekani inaendelea kushuka na shilingi kuongezeka thamani.
Sekta ya utalii kwa kipindi cha miaka mitano ya utawala wake imefanya vizuri. Hivi sasa Pato la Utalii linachangia asilimia 17 ya Pato la Taifa (DGP), huku ikiingiza fedha za kigeni ni asilimia isiyopungua 25, ambazo nia ya serikali ya Rais Samia imepanga kuingia zaidi ya watalii Milioni tano na kufanya asilimia ya sasa kuwa juu.
Rais Samia amefungua nchi kwa kulegeza masharti katika uwekezaji wa viwanda na madini, anaendelea kuunganisha sekta isiyo rasmi na Serikali kufanya kazi pamoja, amefanikiwa kuweka ufanisi kwa walipa kodi kwa kulipa bila mitulinga.
Sera za ubinafsishaji zilizoanza wakati wa Serikali ya Awamu ya Pili, chini ya marehemu Mzee Ali Hussein Mwinyi ameziboresha ikiwemo Bandari, ambapo kuna tija kubwa.
CCM isikubali hadithi ya mtu aliyepata bahati ya kuokota almasi akatokea mwingine akamwambia kuwa amewaokota chupa, hivyo alimshauri aitupe, baadaye aliyemshauri akamzunguka na kuichukua. Mama Samia ni bidhaa inajiuza kwa ubora wake ndani na nje ya nchi, anahitaji kupewa ngwe nyingine.